Nyota wetu watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Nyota hao ni mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe walinzi wa kati, Henock Inonga na Joash Onyango.
Kiungo mkabaji Sadio Kanoute na mlinzi wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ waliingia katika tano bora kabla ya kupunguzwa na kubaki watatu.
Mchanganuo wa takwimu zao:
Mechi | Dakika | Goli | Assist | |
Kapombe | 6 | 540 | 1 | 0 |
Henock | 4 | 360 | 0 | 0 |
Onyango | 4 | 360 | 0 | 0 |
Zoezi la kupiga kura tayari limeanza kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa kesho Mei 2 saa sita usiku.
Mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Unaweza kupiga kura yako hapa chini:
One Response
Kazi iendelee