Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya kikosi chetu hadi mwaka 2025.
Tangu alivyorejea kwa mara ya pili mwaka 2017 kutoka Azam FC, Kapombe amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza mpaka sasa licha ya kupita makocha tofauti.
Licha yakuwa mchezaji muhimu ndani ya timu sifa yake nyingine kubwa Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wenye nidhamu hivyo ni mfano wa kuigwa na vijana.
Pamoja na zoezi la usajili wa wachezaji wapya kuendelea lakini tunawaongeza mikataba nyota wetu ambao bado tunahitaji huduma zao.
Benchi la ufundi chini ya kocha, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ limesema linahitaji huduma ya Kapombe na Menejimenti imetimiza takwa hilo kwa kumuongezea mkataba mpya.