Kapombe akabidhiwa tuzo yake na Emirate Aluminium ACP

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Februari wa mashabiki (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kapombe amewapiku winga Peter Banda na mlinzi wa kati Henock Inonga ambao aliingia nao fainali katika kinyang’anyiro hicho. Katika mwezi Februari amecheza mechi nne amefunga moja na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Kapombe amewashukuru Wadhamini Emirate Aluminium ACP kwa kutoa motisha ambayo inawafanya wachezaji kujituma kuisaidia timu.

“Kwanza niwashukuru Emirate kwa kudhamini tuzo hii, inaongeza morali kwetu kama wachezaji. Pia niwashukuru wachezaji wenzangu kwa ushiriakiano mkubwa walionipa.

“Kwangu hii ni changamoto ambayo inanifanya niendelee kujituma kwa ajili ya kuisaidia timu kufanya vizuri na ndio lengo la kila mchezaji wa Simba,” amesema Kapombe.

Afisa Uhusiano wa Emirate Aluminium ACP, Isaa Maeda amewaomba watu waendelee kununua bidhaa za ujenzi za kampuni hiyo ambapo kwa sasa wameleta taa za kisasa.

“Nawaomba watu waendelee kununua bidhaa zetu, tumekuja na bulb (taa) pia ambazo ni kama mapambo kwenye nyumba. Tunawaomba Watanzania kuboresha maisha yao kwa kununua bidhaa zetu,” amesema Maeda.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER