Kapombe afunguka faida ya mchezo wa marudiano dhidi ya Raja

Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Machi 31 kwa saa za Morocco utakuwa na faida kwetu mara mbili.

Kapombe amesema kwakuwa tayari tumefanikiwa kutinga robo fainali tutautumia mchezo dhidi ya Raja kama sehemu ya maandalizi kuelekea hatua inayofuata.

Kapombe ameongeza kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo tayari yameanza na wachezaji wanaendelea na mazoezi kujiweka sawa.

“Mchezo utakuwa mgumu, Raja ni timu kubwa Afrika na tunaenda kwao. Tayari tumefanikiwa kutinga robo fainali hivyo tutautumia mchezo dhidi ya Raja kama sehemu ya maandalizi sababu ni mechi ya mwisho ya kundi,” amesema Kapombe.

Kapombe amewashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kuisapoti timu katika hali zote na wamekuwa na mchango mkubwa kuifikisha robo fainali.

“Mashabiki wamefanya kazi kubwa mpaka kufika sasa, tunaendelea kuwasisitiza wasichoke mapambano yanaendelea na tumeingia robo fainali bado tunahitaji sapoti yenu nasi kama wachezaji tupo tayari kuwalipa furaha,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER