Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amecheza mchezo wake 100 wa Ligi Kuu tangu alipojiunga nasi kwa mara ya pili akitokea Azam FC mwaka 2017.
Tangu alipotua Simba, Kapombe amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza na amejihakikishia namba upande wa kulia.
Kapombe anakuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi za ligi kwa waliopo kikosini kwa sasa.
Kwa mujibu wa takwimu Kapombe amefunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa mengine 25 kwenye ligi tangu ajiunge nasi mwaka 2017.