Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo nyota Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.
Kapama ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kama beki, kiungo na mshambuliaji hali iliyolivutia benchi la ufundi na kumsajili.
Akiwa Kagera Sugar msimu uliopita Kapama amefunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu baada ya kucheza mechi 25.
Kabla ya kujiunga na Kagera Kapama alikuwa akicheza Ndanda FC.