Kanoute, Sakho, Inonga kuchuana Mchezaji Bora wa Mashabiki Januari

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute, kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho na mlinzi wa kati Henock Inonga ndiyo waliofanikiwa kuingia fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Ndani ya mwezi Januari, Kanoute amecheza mechi saba sawa na Sakho huku Inonga akicheza nane huku wote wakionyesha kiwango bora.

Zoezi la mashabiki kupiga kura litaanza leo saa 12 jioni kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Jumatano Februari 2 saa 10 jioni.

Mshindi wa jumla atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa Wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Kiungo Jonas Mkude ndiye aliyechukua tuzo hiyo mwezi Desemba huku Bernard Morrison akinyakua Novemba.

SHARE :
Facebook
Twitter

66 Responses

  1. Kazi nzuri sana inafanywa na viongozi wa Simba,Siku hizi tumebadilika kabisa kisoka tofauti na tulipotoka,Haya matokeo ya hapa kati ni matokeo tuu ya mchezo wa mpira wa miguu Hivyo isitukatishe tamaa nawasihi waendelee na mipaƱgo mizuri ya timu yetu.Pia naomba hii website izid kuboreshwa!SIMBA NGUVU MOJA

    1. Tunapiga kura sehemu gani sasa? Huyo tuzo apewe P. O. Sakho ameonesha kiwango kikubwa kwenye Mapinduzi Cup na hata mechi za hivi karibuni

  2. Huu mfumo wa kupiga kura ufanyiwe maboresho mana hauko stable unayumba kiasi cha watu kushindwa kupiga kura

  3. Ndio mchezaji ambaye amezuia wachezaji wa timu pinzani wasionyeshe makali kwenye lango la timu yetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER