Kanoute Mchezaji bora wa Mashabiki Novemba

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Novemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month Month).

Kanoute ambaye amekuwa mhimili kwenye kikosi amewashinda Mzamiru Yassin na Shomari Kapombe ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Kanoute ameshinda tuzo hii kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na kikosi chetu msimu uliopita lakini mara kadhaa ameingia tatu bora.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Kura Asilimia

1. Kanoute 319 43.11

2. Mzamiru 240 32.43

3. Kapombe 181 24.46

Katika mwezi Novemba Kanoute amecheza mechi tano sawa na dakika 398 akiwa hajafunga wala kutoa asisti lakini ameonyesha kiwango bora.

Kama ilivyo kawaida Kanoute atakabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile ikiwa ni sehemu ya zawadi ya kuibuka mshindi wa kinyang’anyiro hicho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER