Kanoute, Bwalya, Dilunga wachuana Mchezaji Bora Simba

Nyota watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Oktoba wa mashabiki ya Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month.

Emirate Aluminium ACP wamekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wachezaji.

Wachezaji hao ni viungo Sadio Kanoute, Rally Bwalya na Hassan Dilunga ambao wamekuwa kwenye kiwango bora katika mwezi huo.

Awali walikuwa wachezaji watano akiwamo mlinda mlango Aishi Manula na Bernard Morrison kabla ya Kamati maalumu kuwachuja na kubaki na hao watatu ambao wameingia fainali.

Mshindi kati ya watatu hao atapatikana kupitia kura za mashabiki zitakazopigwa katika tovuti rasmi ya klabu ya www.simbasc.co.tz

Zoezi la kupiga kura limeanza leo na litakamilika Jumatano saa 10 jioni na mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

This poll has ended (since 2 years).
SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Naomba makocha wamwamini doncan nyoni Kama wing back pamoja na yusuph mhiru, na wengine Kama yule aliyesajiriwa kutoka gwambina fc. Pia sub zisifanyike dakika ya 8O’s fanya dakaika ya 60’s Kama matokeo yameshakuwa magumu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER