Kiungo mkabaji Sadio Kanoute amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Novemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Kanoute ambaye ndiyo mara yake ya kwanza kuchukua tuzo hiyo tangu ajiunge na kikosi chetu amewapiku kiungo mkabaji Mzamiru Yassin na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.
Katika mwezi Novemba, Kanoute amecheza mechi tano sawa na dakika 398 akiwa hajafunga wala kutoa assist lakini ameonyesha kiwango bora na kuwa muhimili wa timu.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Kanoute amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa pamoja na mashabiki waliompigia kura na kumefanya kuibuka na ushindi.
“Kwanza niwashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano mkubwa pamoja na mashabiki walionipigia kura, tuzo hii imenipa deni ya kunifanya niendelee kupambana kwa ajili ya timu,” amesema Kanoute.
Kanoute amekabidhiwa fedha taslimu Sh milioni mbili na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi ya kushinda tuzo hiyo.