Kiungo mkabaji, Sadio Kanoute amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya yamekamilika.
Kanoute amesema kabla ya kuwasili nchini Guinea jana walifanya mazoezi kwa siku tatu jijini Dar es Salaam hivyo wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo.
Kanoute amesema wachezaji wanajua utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wenyeji hasa kwakuwa wapo nyumbani lakini tupo tayari kuwakabili.
“Tumejianda vizuri na mchezo, tulianza maandalizi siku atu zilizopita tunajua mchezo utakuwa mgumu, Horoya ni timu nzuri ila sisi ni Simba na tumejipanga kufanya vizuri.”
“Sisi kama wachezaji tupo vizuri na kocha ametuandaa kiakili na kimwili tayari kwa ajili ya mechi ya kesho, itakuwa vizuri kama tutapata ushindi ugenini,” amesema Kanoute.