Kampeni ujenzi wa uwanja yazinduliwa

Klabu yetu leo imezindua rasmi kampeni ya kuchangisha fedha za kujenga uwanja wetu wa kisasa kwa ajili ya mechi zetu za nyumbani.

Wikiendi iliyopita Rais wa Heshima ambaye ni mwekezaji wa klabu, Mohamed Dewji (Mo) aliishauri Bodi ya Wakurugenzi kutangaza utaratibu wa kuchangisha wanachama na mashabiki huku yeye akiahidi kutoa Sh bilioni mbili kufanikisha ujenzi huo.

Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez wamezindua kampeni hiyo leo mbele ya wanahabari ambayo imepewa jina ‘SIMBA YETU UWANJA WETU’ kwa ajili ya kuhamasisha watu kuchangia.

Wanachama na mashabiki watachangia pesa kupitia mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom, Airtel na benki ya NMB ambapo namba za kutumia tayari zimewekwa hadharani.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

 1. HONGERA Simba Sc na Uongozi wote wa Klabu kwa kuanza kampeni ya ujenzi wa uwanja. Mimi ni mshabiki wa hii klabu kwa kuzaliwa.
  Pendekezo langu na matamanio yangu ni kuona uwanja unaojengwa uwe na uwezo wa kuchukua angalao watazamaji 55,000 AU HATA ZAIDI (na sio 30,000).
  Sababu ya kupendekeza ni:
  i. Uwanja huo utaishi si chini ya miaka 50
  ii. Klabu ya Simba inazidi kukua na kuongeza washabiki mpaka nje ya mipaka ya nchi yetu (mf. Morison kabla ya kujiunga na timu yetu)
  iii. Tunaweza kujenga jukwaa moja baada la lingine hata kama itachukua muda kiasi
  iv. Vinginevyo kama ni lazima kuwa wa watazamaji 30,000 basi mfikirie uwanja wa majukwaa ya muda (ya kuhamishika) kama nilivyosikia viwanja vinavyojengwa huko Qatar kwa ajili ya kombe la dunia mwakani (wamesema baada ya mashindano watavitoa kwa wadau wengine popote duniani ili kuendeleza soka
  v. Nina shaka uwanja unaweza kupitwa na wakati miaka 2 baada ya kwisha kwa kuwa utaonekana mdogo
  vi. Baada ya kujenga hayo majukwaa ya kudumu hatutakuwa na nafasi tena ya kuongeza ili kubeba washabiki wengi zaidi ya hao 30,000

  SIMBA IS AT NEXT LEVEL, PLEASE THINK BIG

  Semndili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER