Kamati ya Maboresho ya Katiba yataja hatua tuliyofikia

Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Katiba, Hussein Kitta amesema mambo sita ambayo tulielekezwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuyafanya ili tuweze kukamilisha mchakato wa uendeshaji mpya wa Klabu njia ya hisa umekamilika.

Kitta amesema baada ya kuona mchakato umechukua muda mrefu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro alituita Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), BMT na Taasisi ya Usajili Vizazi na Vifo (RITA) ili kujadili kinacho kwamisha na kila pande ilielezea.

Kitta ameongeza kuwa baada ya kikao hicho ndipo tukatakiwa kufanya marekebisho ya mambo sita yaliyopo kwenye katiba ya zamani ili tuendane utaratibu tulioagizwa na Serikali na hilo pia limefanyika na kukamilika.

“Kamati yangu imekuwa na vikao mbalimbali ya kuhakikisha haya maboresho ya katiba  yanafanyika kwa muda kama tulivyoelekezwa na BMT na tayari tumekamilisha.

“Na marekebisho yote yaliyotakiwa kufanywa mnufaika mkubwa ni Simba na BMT ilituagiza tupeke rasimu waipitie kabla ya kuipeleka kwa wanachama na tumefanya hivyo na jambo jema ni kwamba wameipitisha na tumepewa ruhusa ya kuendelea na mchakato,” amesema Kitta.

Kitta amesema maboresho haya yatapelekwa katika mkutano mkuu wa klabu utakaofanyika Jumapili Januari 21 kwa ajili ya kupitishwa kwenye katiba ili mchakato wa uendeshwaji wa klabu kwa mfumo wa hisa uendelee.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER