Kakolanya afurahia ‘clean sheet’

Mlinda mlango namba mbili, Beno Kakolanya amefurahi kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi msimu huu bila kuruhusu kufungwa bao (clean sheet).

Mchezo huo uliopigwa jana dhidi ya Biashara United na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, ni wa kwanza kwa Kakolanya kudaka msimu huu wa 2021/22.

Pamoja na mambo mengine, Kakolanya hakusita kumsifia Kocha wa Makipa, Tyrone Damons raia wa Afrika Kusini kwa kazi kubwa anayoifanya kuwafundisha hatua inayowafanya kujiamini wakiwa langoni.

“Najisikia vizuri kupata nafasi ya kucheza, najisikia furaha kuisaidia timu yangu kupata pointi tatu muhimu na pia nimefurahi kupata clean sheet, hii ndiyo mechi yangu ya kwanza ya ligi msimu huu.

“Namshukuru kocha wetu wa makipa Tyrone kwa kazi kubwa anayofanya kwetu ndiyo maana unaona tunakuwa bora na kujiamini langoni. Kocha ametuongezea vitu vingi katika vipaji,” amesema Kakolanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER