Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Red Arrows

Mshambuliaji Medie Kagere amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa keo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Kagere atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo watatu washambuliaji ambao ni Rally Bwalya, Bernard Morrison na Hassan Dilunga.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi Kocha Pablo Franco amewapanga Jonas Mkude na Sadio Kanoute huku Joash Onyango na Pascal Wawa wakisimama kama mabeki wa kati.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5),
Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6)
Jonas Mkude (20), Hassan Dilunga (24), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Bernard Morrison (3)

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Erasto Nyoni (18),
Henock Inonga (29), Mzamiru Yassin (19), Peter Banda (11),
Ibrahim Ajibu (10), John Bocco (22) na Duncan Nyoni (23).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER