Kocha Didier Gomes leo ameamua kuanza na washambuliaji wawili Medie Kagere na John Bocco katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United itakayopigwa Uwanja wa Karume mkoani Mara saa 10 jioni.
Mara nyingi Gomes amekuwa akipendelea kumtumia mshambuliaji mmoja na kuweka viungo watatu wa ushambuliaji hasa katika mechi za nyumbani.
Nahodha Bocco na Kagere wataanza pamoja kutokana na wapinzani Biashara kutumia nguvu hasa katika idara yao ya ulinzi.
Israel Patrick naye ataanza katika mchezo wa leo akichukua nafasi ya Mohamed Hussein huku Henock Inonga akipangwa kiungo wa ulinzi akichukua nafasi ya Taddeo Lwanga ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Rally Bwalya (8), Erasto Nyoni (18), Medie Kagere (14) John Bocco (22)
Hassan Dilunga (24).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Mohamed Hussein (15), Mzamiru Yassin (19),
Pape Sakho (17), Peter Banda (11),
Duncan Nyoni (23), Chris Mugalu (7), Yusuph Mhilu (27), Jimmyson Mwinuke (21).