Kagere arejesha furaha dakika za majeruhi

Bao lililofungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika za majeruhi kabla ya kipenga cha mwamuzi limetuwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kagere alifunga bao hilo akiwa ndani ya 18 dakika ya nyongeza baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Chris Mugalu.

Bernard Morrison alitupatia bao la kwanza dakika ya 39 baada ya mlinzi wa Coastal kumgongesha mpira katika jitihada za kupiga mbele na kuumalizia wavuni.

Victor Akpan aliisawazishia Coastal bao hilo dakika ya 77 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango Aishi Manula.

Dakika ya 87 Nahodha wa Coastal Pascal Kitenge alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Kibu Denis, Sadio Kanoute na Taddeo Lwanga na kuwaingiza Yusuf Mhilu, Jonas Mkude na Medie Kagere.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha alama 40 tukiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya wanaongoza tukiwa na faida ya mechi moja mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER