Kaduguda auota ubingwa wa Shirikisho Afrika

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Mwina Kaduguda ameweka wazi kuwa lengo letu msimu huu liwe kuchukua taji la Kombe la Shirikisho Afrika ili tuvunje rekodi yetu kwa kuwa tuliwahi kufika fainali.

Kaduguda amesema mwaka 1993 tuliingia fainali ya michuano hii tukafungwa na Stella Abidjan kutoka Ivory Coast kwa hiyo tunapaswa kuvunja rekodi kwa kuchukua ubingwa wakati huu.

Kaduguda ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu ameongeza kuwa wapinzani wetu Orlando Pirates si timu ya kubeza wamewahi kuchukua taji hilo mwaka 1995 hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari.

“Kama kunahitajika mtu afe ili Simba ichukue ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mimi nipo tayari kufanya hivyo halafu nikifika huko naenda kufungua tawi akhera. Tumewahi kufika fainali Kwahiyo tunapaswa kuvunja rekodi kwakuchua ubingwa,” amesema Kaduguda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa zamani wa klabu, Hassan Dalali amewasisitiza wachezaji waone umuhimu mchezo na wajitoe kuipigania timu Jumapili ili kuwapa furaha Wanasimba.

“Wachezaji wanapaswa kujua thamani ya timu, sisi mashabiki tunahitaji furaha. Tunaweza kuifunga Orlando kama kila mchezaji atatimiza majukumu yake uwanjani,” amesema Dalali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER