Jumapili tunakuja na ‘Wenye Nchi Beach Party’

Baada ya kutumia njia mbalimbali za hamasa kuelekea mechi zetu za Ligi ya Mabingwa Afrika safari hii tumekuja tofauti Jumapili tutakuwa Coco Beach na itakuwa ‘Wenye nchi Beach Party’.

Hii itaanza saa nne asubuhi mpaka saa 11 jioni ambapo burudani mbalimbali zitakuwepo Wanasimba kutoka maeneo yote wanakaribishwa.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema shughuli zote tunazofanya katika mikutano ya hamasa zitakuwepo kama kuuza tiketi na kuuza jezi zitakuwepo.

“Sisi ndio waanzilishi wa kila kitu, safari hii ‘kispika kitakuwa Coco Beach Jumapili. Tumeshaenda Masokoni, Feri, Vituoni na kila mahali tumewafikia Wanasimba sasa tunakutana Coco Beach.

“Jumapili itakuwa ni Wenye Nchi Beach Party’ tunakula bata tunafurahi, tunanunua tiketi na jezi kwa ajili ya Vipers Jumanne,” amesema Ahmed.

Ahmed amesema ratiba ya Jumatatu itakuwa mashabiki kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mazoezi ya mwisho kabla ya kuingia mitaa ya Temeke na viunga vyake kuendelea na hamasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER