Jumanne tunakuja na ‘Nguvu Moja kwa Mkapa Hatoki Mtu’

Kama ilivyo kawaida kila tunapoelekea katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika hasa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tunakuwa na slogan mbalimbali ili kuongeza hamasa kwa mashabiki.

Kuelekea mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne saa moja usiku tumekuja na ‘slogan’ ya ‘Jumanne ya wenye nchi, Nguvu Moja kwa Mkapa hatoki mtu’.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema tunajua Jumanne ni siku ya kazi lakini Wanasimba wana mapenzi makubwa na timu yao haijalishi ni muda gani inacheza.

“Ni kawaida yetu kuwa n ‘slogan’ tofauti,  kuelekea mchezo wetu dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumanne, safari hii tunasema ‘Jumanne ya wenye nchi, Nguvu Moja kwa Mkapa Hatoki Mtu’.

“Tunajua Vipers ni timu nzuri na imewahi kuja kwa Mkapa na ikashinda lakini hawajawahi kukutana na ‘vibes’ la Wanasimba kwahiyo wajiandae na pumzi ya moto,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER