Jumamosi ni Vita ya Kisasi dhidi ya Jwaneng Galaxy

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally ametangaza kuwa kauli mbiu ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumamosi ni Vita ya Kisasi.

Ahmed amesema lengo la kauli mbiu hiyo ni kutaka kulipa kisasi kutokana na Jwaneng Galaxy kwakuwa waliwahi kututoa katika hatua kama hii nasi tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

Aidha Ahmed amesema vita hii haipaswi kupiganwa na wachezaji pekee au viongozi bali kila Mwanasimba hivyo mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi.

“Tunakumbuka mwaka 2021 Jwaneng walitutoa kwenye michuano hii, ndio maana tunasema ni Vita ya Kisasi kwakuwa tunataka kuwapa huzuni Jwaneng kama walivyofanya kwetu.”

“Faida ya kushinda katika mchezo dhidi ya Jwaneng ni tatu ambazo ni kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tunakuwa tumelipa kisasi na tunakuwa timu ya tano kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya nne mfululizo,” amesema Ahmed

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER