Joshua Mutale ni Mnyama

Kiungo mshambuliaji Joshua Mutale raia wa Zambia amejiunga na kikosi chetu baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Power Dynamos ya Nchini kwao.

Mutale mwenye miaka 22 anamudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani tena kwa ufanisi wa hali ya juu.

Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia, kushoto na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.

Akiwa Power Dynamos msimu uliopita, Mutale amefunga mabao manane na kuisaidia kupatikana kwa mengine m katika michezo 26.

Uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi nyingi Uwanjani pamoja na umri ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kumsajili mchezaji huyo ikiwa ni mkakati maalumu wa kuboresha kikosi chetu kwa kusajili damu changa na wenye ubora

Joshua Mutale anakua ni mchezaji wa pili kusajiliwa ndani ya Simba baada ya Lameck Lawi na bado Wachezaji wengine wataendelea kusajiliwa na kutambulishwa

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER