Kiungo mshambuliaji, Jimmyson Steven Mwanuke amejiunga na timu yetu kutoka Gwambina FC tayari kwa ajili ya kampeni za msimu mpya wa ligi.
Mwanuke ni mmoja wa wachezaji vijana mwenye uwezo mkubwa na anatarajiwa kuwa hazina kubwa kwa taifa katika siku za usoni.
Nyota huyo ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi za ushambuliaji tayari yupo nchini Morocco na wenzake kujiandaa na msimu mpya.
Uwezo mkubwa alioonyesha akiwa Gwambina ndiyo uluosababisha benchi la ufundi kumpendekeza kwa uongozi kabla ya kusajiliwa.
Msimu huu tumeamua kufanya usajili wa kisayansi na kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi sababu dhamira yetu ni kutetea ubingwa wa ligi, FA na kuvuka robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.