Jezi zenye majina ya Viongozi zatambulishwa kileleni

Tumefanikiwa kuzindua jezi zetu ambazo tutazitumia kwenye mashindano mbalimbali msimu ujao kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kwenye jezi hizo tumeandika majina mgongoni ya Viongozi wa wakuu wa Serikali ikiwa ni kuthamini mchango wao.

Jezi hizo ambazo zimezinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ina majina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi na Makamo wa Rais, Dk. Phillip Mpango.

Nyingine zimeandikwa majina ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson na Rais wa Heshima wa klabu Mohamed Dewji ‘Mo’.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula ameweka wazi kuwa baada ya jezi hizo kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro zitapigwa mnada na pesa zitakazopatikana zitajenga Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa Zanzibar.

Kajula amesema kile Kibegi kilichotumika kubebeza jezi hizo kitapelekwa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kutokana na umaarufu kilichojizolea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER