Jefferson Luis ni Mnyama

 

Mlinda mlango, Jefferson Luis Szerban (29) raia wa Brazil amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.

Jefferson tumemsajili kutoka klabu ya Resende FC kutoka Brazil msimu uliopita ameichezea Itabirito FC-MG kwa mkopo.

Tayari mlinda mlango huyu ameungana na kikosi nchini Uturuki kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu wa mashindano 2023/24 akitokea Brazil.

Jefferson ana uwezo mkubwa wa kulinda lango huku akitumia miguu yote kwa ufasaha pamoja na kumudu kuanzisha mashambulizi.

Jefferson ambaye ana urefu wa futi 1.92 anakuja kuungana na walinda milango, Aishi Manula, Ally Salim na Ahmed Feruzi ‘Teru’.

Jefferson ana uzoefu wa kucheza mechi nyingi za ushindani hivyo tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu hasa ukizingatia Manula atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER