Jambo letu kwa Mkapa leo ni pointi tatu tu…

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuikabili RS Berkane kutoka Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo jambo pekee tunalohitaji ni kupata pointi tatu nyumbani.

Katika michuano hii ya Afrika kila timu inatumia uwanja wa nyumbani kuhakikisha inapata pointi tatu hatua ambayo tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha leo.

Tutaingia katika mchezo wa leo kwa tahadhari zote kwa kuwa tunajua Berkane ni timu nzuri na ilitufunga kwao nasi tunahitaji kushinda nyumbani.

PABLO AFUNGUKA

Kocha Mkuu Pablo Franco amesema mchezo wa leo muhimu kwetu na utaamua mustakabali wetu kwa namna yoyote hivyo tukiwa nyumbani mbele ya mashabiki tunapaswa kushinda.

Pablo amesema tuna uzoefu mkubwa wa kucheza mechi katika uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki na tumejipanga kuhakikisha tunatumia nafasi tutakazo tengeneza kupata mabao.

Pablo ameongeza kuwa kikosi kimepata wiki moja ya maandalizi na mapumziko ya siku moja hivyo wachezaji wapo katika hali nzuri tayari kwa kupambana kutafuta ushindi.

“Tunafahamu tunaenda kukutana na timu bora ambayo ilitufunga kwao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kwetu.

“Tumepata muda mzuri wa kujiandaa, tulikuwa na wiki ya kufanya mazoezi wachezaji wapo kwenye hali nzuri tunaamini tutafanya vizuri,” amesema Pablo.

WACHEZAJI WAWAITA MASHABIKI

Nyota wetu wamewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kutupata sapoti kwa kushangilia na hatimaye tubakishe alama tatu muhimu nyumbani.

Mlinda mlango Aishi Manula, nahodha msaidizi, Mohamed Hussein na kiraka, Erasto Nyoni kwa nyakati tofauti wamesisitiza kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani katika mchezo wa leo.

KIBU NDANI

Mshambuliaji Kibu Denis ambaye usajili wake wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ulichelewa sasa kila kitu kipo sawa na kama benchi la ufundi litaona inafaa anaweza kutumika kwenye mchezo wa leo.

Kibu ambaye alikuwa majeruhi muda mrefu katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji aliingia kipindi cha pili na kuonyesha uwezo mkubwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER