Israel aiita mechi dhidi ya Al Hilal ‘Ya Wakubwa’

Mlinzi wa kulia Israel Patrick amesema mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya wenyeji Al Hilal ni ya wakubwa kutokana na kukutanisha timu zenye historia kubwa.

Israel amesema sisi ni timu yenye historia kubwa Tanzania kama ilivyo kwa Hilal hapa Sudan kwa hiyo mchezo lazima utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Mlinzi huyo ameongeza kuwa kwa upande wao wa wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

“Tunategemea mchezo mgumu kutoka kwa Hilal, wao ni timu kubwa hapa Sudan kama tulivyo sisi kule nyumbani kwa hiyo ni mchezo unaokutanisha wakubwa tupo tayari kucheza kikubwa.

“Hali ya hewa haina tofauti kubwa na ile ya nyumbani hivyo hatutegemei kupata changamoto yoyote kwenye hilo, tunategemea kupambana kupata ushindi,” amesema Israel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER