Mlinzi wa kati, Henock Inonga amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Februari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Inonga amewashinda mlinzi wa kulia Shomari Kapombe na kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin ambao ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Katika mwezi Februari, Inonga amecheza mechi zote tano, tatu za Ligi ya Mabingwa na mbili za ligi kuu sawa na dakika 450 akifunga bao moja.
Mchanguo wa kura zilivyopigwa na mashabiki kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz.
Kura Asilimia
Inonga 498 57.97
Kapombe 246 28.64
Mzamiru 115 13.39
Hii ni mara ya pili kwa Inonga kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki, msimu uliopita pia alifanikiwa kuinyakua.
Inonga atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000, 000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile ikiwa ni zawadi ya kuibuka mshindi.