Inonga, Chama waitwa timu zao za taifa

Nyota wetu wawili wa kimataifa mlinzi Henock Inonga na kiungo mshambuliaji Clatous Chama, wameitwa kwenye timu zao za taifa kujiandaa na mechi mbili za kalenda ya FIFA.

Inonga amejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Congo DR inayonolewa na Kocha Sebastian Desebre ambapo itacheza mechi mbili dhidi ya Burkina Faso na Sierra Leone.

Inonga ambaye ni beki bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita ndiye mchezaji pekee anayecheza ligi ya Tanzania kuitwa kwenye kikosi hicho.

Kwa upande wa Chama amejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambacho kitacheza mechi mbili dhidi ya Libya na Mali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER