Inonga, Baleke ndani ya Kikosi Bora cha CAF

Mlinzi wa kati, Henock Inonga na mshambuliaji Jean Baleke wamejumuishwa katika Kikosi Bora cha Wiki cha Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wawili hao wamepata alama nyingi kutokana na ubora waliouonyesha katika mchezo uliopita uliofanyika Juzi Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam dhidi ya Wydad Casablanca ambapo tuliiibuka na ushindi wa bao moja.

Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji wetu kujumuishwa kwenye kikosi bora cha wiki kutokana na viwango wanavyoonyesha kwenye kila mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER