Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili na mlinzi wa kati, Henock Inonga Baka ambao utamuweka klabuni hadi mwaka 2025
Mkataba wa awali wa Inonga unamalizika mwishoni mwa msimu huu yaani 2023 na leo ameongezewa mkataba mwingine miaka miwili ambapo ataendelea kusalia klabuni hadi 2025.
Kumekuwa na taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali ya kuwa mkataba wa Inonga yu mbioni kuondoka Simba jambo halina ukweli wowote.
Inonga ndiye beki bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita na beki bora wa nchini DR Congo.
Katika dirisha hili dogo la usajili Uongozi umedhamiria kuboresha kikosi kwa kuongeza wachezaji wapya kama ilivyopendekezwa kiufundi sanjari na kuwaongezea mikataba wachezaji wote ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.
Uongozi unaendelea kuwasisitiza wanachama, wapenzi na mashabiki kufuatilia taarifa rasmi zinatolewa na klabu kupitia kurasa zetu.