Inonga atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora

Mlinzi wa kati Henock Inonga, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Ndani ya mwezi Aprili, Inonga amecheza mechi nne sawa na dakika 360 huku akionyesha kiwango safi kwenye michezo yote.

Inonga amewapiku walinzi wenzake Shomari Kapombe na Joash Onyango ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Baada ya kuibuka mshindi, Inonga atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

Jina Kura Asilimia

Kapombe 457 16.49
Inonga 2277 82.14
Onyango 38 1.37

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER