Inonga arejea kikosini

Mlinzi wa kati Henock Inonga amerejea kikosini baada ya kumaliza majukumu ya timu yake ya Taifa ya DR Congo iliyokuwa inashiriki michuano ya AFCON iliyomalizika nchini Ivory Coast wiki iliyopita.

Henock ameshiriki mazoezi ya jioni pamoja na wenzake ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Kurejea kwa Inonga kunafanya kikosi chetu kuwa kamili maana hakuna mchezaji ambaye hajajiunga na wenzake.

Kikosi kimerejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya siku moja kufuatia ushindi wa bao moja dhidi ya JKT Tanzania tuliopata siku ya Alhamisi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER