Inonga aisaidia DR Congo kutinga nusu fainali AFCON

Mlinzi wetu wa kati Henock Inonga amekuwa muhimili mkubwa katika kuisaidia timu yake ya DR Congo kutinga nusu fainali ya michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.

Inonga amecheza dakika zote 90 katika mchezo wa jana wa robo fainali dhidi ya Guinea ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kocha Mkuu wa DR Congo, Sebastien Desabre amekuwa akimuamini Henock katika idara ya ulinzi wa kati pamoja na nahodha Chancel Mbemba.

Simba inaendelea kumuombea Inonga azidi kufanya vizuri na kuisaidia nchi yake ikiwezekana kutwaa taji la AFCON.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER