Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino ameipongeza timu yetu ya Simba Queens kwa kufanikiwa kuibuka na ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake 2023/24.
Infantino ametuma salamu hizo kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuzifikisha kwetu.
Infantino amesema juhudi tulizofanywa kwa msimu mzima zimezaa matunda na hilo ni jambo la kupongezwa.
Aidha Infantino ameupongeza Uongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki kwa kufanikisha kupatikana kwa ubingwa huo.