Imani Kajula ndiye CEO wetu mpya

Uongozi klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri Ndugu Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)

Kajula anachukua nafasi iliyoachwa na Barbara Gonzalez ambaye alijiuzulu nafasi hiyo Desemba 10, 2022.

Kajula ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyofanyika nchini mwaka 2019.

Kabla ya kujiunga nasi Kajula alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu 2013 mpaka sasa.

Kajula ni mbobevu wa masuala ya Masoko na Mawasiliano na amefanya kazi na makampuni mbalimbali na mabenki ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa kazi alizofanya mpaka sasa.

– Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB (2006-2013)

– Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta (2003-2006)

– Meneja Masoko wa CRDB (1999-2003)

Akiwa EAG Group Kajula alikuwa sehemu ya maandalizi ya Wiki ya Simba mpaka kilele chake (Simba Day) ambapo kampuni hiyo ndiyo ilitengeneza mitandao ya kijamii ya klabu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER