Huyu hapa Mgeni rasmi mchezo wetu dhidi ya RS Berkane

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Omari Said Shaaban atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tumekuwa na utaratibu wa kualika viongozi mbalimbali wa serikali katika mechi zetu za kimataifa zinazofanyika nyumbani ili kuongeza thamani ya mechi ya husika.

Katika mchezo uliopita dhidi ya ASEC Mimosas tulimualika Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Musa Azzan Zungu.

Mchezo wetu dhidi ya Berkane utaanza saa 10 jioni na maandalizi yanaendelea vizuri na kila kitu kipo mahala pake.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER