Huu hapa uzi mpya wa Mapinduzi, ASFC

Leo tumezindua rasmi jezi mpya ambazo tutazitumia katika Michuano ya Mapinduzi na Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kama kawaida jezi za nyumbani zitakuwa rangi nyekundu na ugenini nyeupe.

Jezi hizo zitaanza kuonekana katika mchezo wetu wa kwanza wa Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Selem View utakaopigwa Jumatano saa 10:15 jioni Uwanja wa Amani.

Tumekuwa na utaratibu wa kuzindua jezi mpya katika mashindano mengine na msimu huu tutazitumia katika Mapinduzi na baadaye ASFC.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER