Hussein Kazi ni Mnyama

Katika kuendelea kufanya maboresho ya kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/24 leo tumefanikiwa kuipata saini ya mlinzi wa kati Hussein Kazi kwa mkataba wa miaka miwili.

Hussein (23) ni kijana mwenye uwezo mkubwa na tunatarajia atakuwa ingizo bora kikosini.

Katika eneo la mlinzi wa kati, Hussein ataungana na wazoefu Henock Inonga, Kennedy Juma na Che Fondoh Malone.

Hussein amecheza soka la kulipwa nchini Shelisheli katika timu ya Forester FC kabla ya kujiunga na Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania na Geita Gold.

Hussein atasafiri usiku wa leo kuelekea Uturuki tayari kijiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya msimu (Pre Season).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER