Duchu: Kambi ya Misri inatujenga

Mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesema kambi yetu ya maandalizi inayoendelea nchini Misri inazidi kuwamairisha kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25. Duchu amesema wachezaji wote wanapambana ili kujiweka sawa ili msimu utakapoanza wawe tayari. Dunchu ameongeza kuwa ushindani wa namba umekuwa mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji wapya waliosajiliwa pamoja na wenyeji. Akizungumzia kuhusu […]

Ni Rasmi tutacheza na Yanga Ngao ya Jamii Agosti 8

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza tutacheza dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 8 saa moja usiku. Mfumo huu wa kucheza Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii ni mara ya pili kutumika ambapo ulianza mwaka jana na tuliibuka Mabingwa […]

Awesu Awesu ni Mnyama

Kiungo mshambuliaji Awesu Awesu amejiunga nasi kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili. Awesu amejiunga nasi akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu. Awesu ni mchezaji mzoefu kwenye Ligi Kuu ya NBC na anaweza kumudu nafasi ya kiungo wa ushambuliaji na winga zote ingawa pia amewahi kutumika […]

Queens wafanyiwa Vipimo vya Afya

Wachezaji wa Simba Queens jana na leo wamefanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/25. Vipimo hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambayo ni damu, mapafu na moyo pamoja na kupima utimamu wa misuli na mishipa. Queens itashiriki mashindano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki (CECAFA) yanayotarajia […]

Kwaheri Pa Omar Jobe

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji Pa Omar Jobe baada ya kipindi kifupi cha miezi sita. Jobe (25) raia wa Gambia amejiunga nasi katika dirisha la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan. Jobe ni mmoja ya […]

LATEST NEWS

FIXTURES

#NGUVUMOJA

Stay up to date with Simba Sports Club

THE CLUB
TEAMS
ACADEMY
FAN ZONE
SHOP

© 2022 Simba Sports Club | Website Administration by Kinara Technologies