Ahoua apiga hat trick tukiichakaza Pamba KMC Complex

Kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa 5-1 tuliopata dhidi ya Pamba Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC. Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 16 kwa mkwaju wa penati baada ya Joshua Mutale kufanyiwa madhambi ndani ya 18. Ahoua alitupatia bao la […]

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Pamba Jiji

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji watano ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania. Fadlu amewaanzisha Mohamed Hussein, Augustine Okajepha, Elie Mpanzu na Leonel Ateba wakichukua nafasi za Valentine […]

Tupo tayari kuikabili Pamba Leo

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Pamba Jiji katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC. Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao moja tuliopata kwenye mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania. Ni moja ya mechi ngumu ambazo tunategemea kukutana nayo kutokana na […]

Simba Queens yaichapa JKT Meja Isamuhyo

Simba Queens imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Wanawake Tanzania (TWPL) baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 4-3 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. JKT walikuwa wakwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 11 kupitia Anastazia Anthony. Jentrix Shikangwa aliisawazishia Queens bao hilo dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati […]

Kauli ya benchi la ufundi kuelekea mchezo dhidi ya Pamba

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba utakaopigwa kesho katika Uwanja wa KMC Complex utakuwa mgumu kutokana nafasi waliyopo wapinzani wetu. Matola amesema Pamba haiko sehemu salama kwenye msimamo hivyo wanatumia nguvu kubwa katika kila mchezo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Matola ameongeza kuwa pamoja na ugumu […]

LATEST NEWS

FIXTURES

#NGUVUMOJA

Stay up to date with Simba Sports Club

THE CLUB
TEAMS
ACADEMY
FAN ZONE
SHOP

© 2022 Simba Sports Club | Website Administration by Kinara Technologies