Hivi ndivyo Queens ilivyomaliza Mzunguko wa kwanza SLWPL

Mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Wanawake Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) umekamilika Februari 15 na timu yetu ya Simba Queens imemaliza ikiwa kinara wa msimamo.

Mpaka mzunguko wa kwanza unakamilika Februari 15 ukijumuisha mechi tisa, Queens tumeshinda tisa na kutoka sare moja na kupoteza moja.

Nahodha wetu Opa Clement ndiye kinara wa ufungaji ambapo  mpaka sasa amefunga mabao tisa huku Jentrix Shikangwa akifunga saba, Asha Djafar akifunga manne.

Takwimu za Queens Mzunguko wa kwanza wa SLWPL

Mechi Ushindi Kupoteza Sare Mabao

9            7            1              1        29

Uwiano wa mabao yetu ni 24 kwa kuwa tumeruhusu matano pekee.

Mchezo wetu wa kwanza wa mzunguko wa pili wa SWPL utakuwa Machi 8 dhidi ya JKT Queens  utakaopigwa Uwanja wa Meja Genarali Isamuhyo.

Mchezo dhidi ya JKT Queens ni wa kisasi kwetu kwa kuwa walitufunga bao moja katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER