Hivi hapa viingilio vya mechi ya marudiano dhidi ya De Agosto

Uongozi wa klabu umeweka hadharani viingilio vya mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Kiingilio cha chini kwenye mchezo huo kitakuwa Sh 3,000 ili kuwapa nafasi ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema tumeweka viingilio hivyo rafiki ili kuwafanya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu kufika hatua ya makundi kwa mara ya nne kwenye historia yetu.

“Tumetangaza viingilio hivi mapema na rafiki ili kuwafanya mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu ikifuzu hatua ya makundi ambayo itakuwa ni mara ya nne,” amesema Ahmed.

Viingilio hivyo vimepangwa kama ifuatavyo

Mzunguko Sh 3,000
Machungwa Sh 5,000
VIP C Sh 10,000
VIP B Sh 15,000
VIP A Sh 20,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER