Hivi hapa Viingilio vya Mchezo wetu dhidi ya Wydad Casablanca

Viingilio vya mchezo wetu wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca tayari vimetangazwa na kile chini kitakuwa Sh. 5000.

Viingilio vipo kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh 5000
Machungwa Sh 10,000
VIP C Sh 15,000
VIP B Sh. 20,000
VIP A Sh. 30,000

Kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga pia kutakuwa na Mnyama Package, Simba Executive pamoja na Platinum.

Mnyama Package: Hizi ni kwa ajili ya kundi la watu, marafiki ambao wangependa kukaa pamoja hivyo tiketi zao zitaanza kuuzwa kwa watu 20. Package hii unaweza kununua tiketi za Mzunguko, VIP A, B na C.

Simba Executive: Hii ni kwa ajili ya Mashirika, Makampuni na Taasisi ambao wangependa wafanyakazi wake kushiriki katika mchezo wetu wa Jumamosi. Tiketi za Executive gharama yake ni Sh. 20,000 kwa mtu mmoja, na ukinunua kuanzia tiketi 20 na kuendelea utapewa kibali cha kuingiza gari yako Uwanjani (Car gate pass).

Platinum: Gharama yake ni Sh.150, 000 ambao watakao nunua tiketi hizi watapata usafiri kutoka Hyatt Regency hadi Uwanjani. Watapata vinjwaji na chakula wakiwa uwanjani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER