Hivi hapa viingilio vya mchezo wetu dhidi ya Horoya Jumamosi

Kiingilio cha chini katika mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya kutoka Guinea utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi kitakuwa Sh. 3000.

Viingilio hivi havina tofauti yoyote ya vile vya mchezo uliopita dhidi ya Vipers kwakuwa lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanavyojitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu.

Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh. 3000

VIP C Sh. 10,000

VIP B Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 150,000

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema tiketi za Executive nazo zitapatikana kwa ajili ya vikundi au makampuni ambayo yatataka kuwanunulia wafanyakazi wake watapelekewa mpaka ofisini kwao.

Tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao, mashabiki wanasisitizwa kununua mapema ili kuepeuka usumbufu siku ya mchezo.

Mchezo wa Jumamosi ni kama fainali kwetu tunahitaji ushindi ili kufuzu hatua ya robo fainali hivyo tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuendeleza moto.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER