Hivi hapa viingilio vya mchezo wa ufunguzi wa AFL

Ufunguzi wa michuano ya African Football League utafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 saa 12 jioni na tayari viingilio vimewekwa hadharani.

Katika ufunguzi huo tutashuka dimbani kuikabili Al Ahly kutoka Misri mtanange ambao tunaamini utakuwa mgumu.

Eneo la VIP A halitauzwa tiketi zake sababu limeandaliwa kwa ajili ya Viongozi mbalimbali kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) pamoja na FIFA.

Hivi hapa viingilio vyenyewe

Platinum Sh. 200,000
VIP B Sh. 40,000
VIP C Sh. 30,000
Orange Sh. 10,000
Mzunguko Sh. 7000

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwenye mtandao na Vituo ziatakapokuwa zinauzwa vitatangazwa muda wowote kutoka sasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER