Hivi hapa viingilio vya mchezo dhidi ya Big Bullets Jumapili

Uongozi wa klabu umeweka hadharani viingilio vya mchezo wetu wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi itakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili saa 10 jioni.

Viingilio hivyo vimeangalia hali halisi ya vipato vya mashabiki wetu ambapo cha chini kitakuwa Shilingi 5,000.

Lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Mkapa kama kawaida yetu tunapocheza michuano ya kimataifa.

Kama kawaida kabla ya kuanza kwa mchezo kutakuwa na burudani mbalimbali ambazo zitaanza kutangazwa wiki hii, jambo la muhimu tunawaomba Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani.

Tumeshinda mchezo wa kwanza ugenini lakini bado hatujafuzu hivyo Wanasimba tunawaomba mjitokeze kwa wingi kuisapoti timu na tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.

Viingilio hivyo ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh 5,000
Machungwa Sh 7,000
VIP C Sh 10,000
VIP B Sh 20,000
VIP A Sh 30,000
Platinum Sh 150,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER