Hitimana kocha mpya Simba

Klabu ya Simba imeimarisha benchi lake la ufundi kwa kumteua Thierry Hitimana (42), kuwa kocha msaidizi wa klabu.

Thierry ni mmoja wa walimu wanaoheshimika nchini Rwanda, ambaye pia amewahi kuwa msaidizi wa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomez, wakati Rayon ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo mwaka 2012.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, amesema Gomez aliipa klabu ombi la kuongezewa msaidizi mwingine kwenye benchi la ufundi na sifa za Hitimana zinakidhi kila kitu.

“Ni jambo la kawaida kwa timu kubwa kuwa na makocha wasaidizi zaidi ya mmoj kutokana na mahitaji ya timu hivyo tumeamua kuongeza nguvu katika timu kwa kuwa na mtu wa aina ya Thierry,” amesema.

Kwa upande wake, Gomez ameeleza kufurahishwa kwake na ujio wa Hitimana aliyesema ni mwalimu wa daraja la juu.

“Wakati nikija Afrika kwa mara ya kwanza nilianzia Rwanda na Rayon ndiyo ilikuwa timu ya kwanza. Nakumbuka nilikuwa mkali sana enzi zile na Hitimana alikuwa anasaidia kupooza joto kidogo. Ni mtu mzuri, ni kocha wa viwango, amesema.

Hitimana ni msomi wa Shahada ya Uzamili katika masuala ya fedha aliyopata nchini Ubelgiji na ana leseni ya ukocha daraja A inayotolewa na CAF.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER