Hiki hapa kikosi kitakachokivaa Azam FC

Medie Kagere na Kibu Denis wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Wawili hao wametengeneza uelewano mzuri baina yao ambacho tayari Kocha Pablo Franco amewaamini kutokana na wanachokifanya uwanjani.

Kagere na Kibu watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Pape Sakho na Rally Bwalya watakaotokea pembeni.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi Kocha Pablo kama kawaida amewaanzisha Jonas Mkude na Sadio Kanoute huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama mabeki wa kati.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8).

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Mzamiru Yassin (19), Hassan Dilunga (24), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Yusuf Mhilu (27)Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. I wish my team all the best in 2022 and from the spirit of our players we are going to bring back trophy🏆🏆🏆

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER