Kikosi chetu leo saa 2:15 usiku kitashuka katika Uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Mlandege katika mchezo wa fainali ya michuano ya Mapinduzi.
Mpaka kufikia leo tayari tumecheza mechi tano tukishinda nne na kutoka sare moja.
Mechi zetu zilikuwa kama ifuatavyo:
Simba 3-1 JKU
Mchezo wetu wa kwanza katika michuano ulikuwa dhidi ya JKU uliopigwa Januari Mosi na tukaibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mabao yetu yalifungwa na Moses Phiri na Saleh Karabaka huku moja wakijifunga wenyewe.
Simba 2-0 Singida Fountain Gate
Mechi yetu ya pili ilikuwa dhidi ya Singida Fountain Gate ambayo ilipigwa Januari tano na tukafanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mabao yetu yalifungwa na Willy Onana pamoja na Luis Miqussone.
Simba 0-0 APR
Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ulikuwa dhidi ya APR kutoka Rwanda ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Tulimaliza hatua ya makundi kwa kuongoza kundi tukiwa na pointi saba.
Robo fainali tulicheza ya Jamhuri.
Katika michuano wa robo fainali uliopigwa Januari nane dhidi ya Jamhuri tuliibuka na ushindi wa bao moja ambalo lilifungwa na Jean Baleke.
Nusu fainali tulicheza na Singida FG
Katika mchezo wa nusu fainali tulikutana na Singida Fountain Gate, Januari 8 na kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati 3-2 kufuatia sare ya kufungana bao moja.
Singida walikuwa wakwanza kupata bao moja kupitia kwa Elvis Rupia dakika ya 11 wakati sisi tulisawazisha kupitia kwa Fabrice Ngoma.
Leo tupo tena Uwanja wa New Amaan kwa ajili ya fainali na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua taji.